NAIVASHA
Muungano wa wasomi wa mji wa Naivasha NPA umesifu namna maafisa wa polisi walidhibiti usalama na kushika doria wakati wa sherehe za disemba na mwaka mpya.
Mwenyekiti wa muungano huo Eskimos Kobia amesema kuwa hakuna visa vyovyote vya utovu wa usalama vilivyoripotiwa kule Naivasha huku wakenya kutoka maeneo mbali mbali wakizuru mji huo.
Naye mwenyekiti wa muungano wa wafanyibiashara wa mji huo Stephen Thuo amesema licha ya idadi ndogo ya watu waliotembelea mji huo ikilinganishwa na miaka ya awali, wale waliofika eneo hilo walisherehekea vya kutosha.
Thuo hata hivyo amesikitika kuwa hali mbaya ya uchumi iliwafanya wengi kutosafiri huku akielezea wingi wa matumaini kuwa mwaka huu mambo yatabadilika.
Leave a Comment