Mwanaume mmoja amekamatwa baada ya kulisogelea jeneza la Malkia Elizabeth II kutoka kwenye msururu wa waombolezaji katika Westminster Hall.
Alikamatwa chini ya sheria ya utulivu wa umma na kupelekwa katika mahabusu, Polisi imesema.
Tukio hilo lilitokea katika bunge majira ya saa nne za usiku Ijumaa , kulingana na taarifa ya polisi.
Matangazo ya video ya moja kwa moja maalum kwa ajili ya tukio la umma kuutazama mwili wa Malkia yalikatizwa kwa kipindi kifupi wakati wa tukio hilo.
Taarifa ya makao makuu ya polisi -Scotland Yard ilisema : “Takriban saa nne za usiku Ijumaa tarehe 16 Septemba, maafisa wa polisi wa ulinzi wa bunge na wa kidiplomasia walimkamata mwanaume katika Westminster Hall kufuatia usumbufu.”
Msemaji wa bunge alisema: “Tunafahamu kuhusu tukio katika Westminster Hall, ambapo mjumbe wa umma alitoka nje ya msururu na kuelekea kwenye jeneza.
Mapema jioni, Mfalme Charles III aliungana na ndugu zake Bintimfalme Anne, Mwanamfalme Andrew na Mwanamfalme Edward, katika mkesha wa maombolezo ndani ya ukumbi.
Marehemu Malkia Elizabeth II atatazamwa na umma katika Westminster Hall hadi siku ya mazishi yake Jumatatu wiki ijayo.
Wakati hayo yakijiri misururu ya kuutazama mwili wa umma imeendelea usiku mzima mjini London, licha ya viwango vya joto kushuka hadi kufikia nyuzijoto 1. Baridi hiyo haikuwazuia maelfu ya watu kuendelea kusimama kwenye misururu kwa ajili ya kuutazama mwili wa Malkia.
masharti ya kuzuia safari za ndege juu ya London na Windsor siku ya Jumatatu ijayo
Mamlaka ya safari za ndege (CAA) inasema hakuna ndege , pamoja na zisile zisizokuwa na rubani (droni) itakayoruhusiwa kupaa chini ya futi 2,500 (au mita 762) juu ya maeneo ambapo ibada itakuwa ikifanyika
CAA inasema marufuku hiyo – ambayo inajumuisha maputo madogo na na tiara- ni muhimu kwa sababu za kiusalama
Leave a Comment