Polisi jijini Nairobi wanamwinda kondakta mmoja aliyeua mwenzake kwa kumdunga kwa kisu kufuatia mzozo wa pesa.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumanne katika mtaa wa Ronald Ngala jijini Nairobi wakati matatu iliyokuwa ikielekea upande wa Githurai 45 ilikuwa inapokea abiria.
Walioshuhudia walisema kuwa kondakta huyo alikuwa anazozania pesa na mwezake kabla ya kuchukua kisu na kumdunga mara kadhaa kifuani na kumuua papo hapo.
Baada ya kutekeleza mauaji hayo kondakta yule anaripotiwa kutoweka asijulikane aliko hadi kufikia sasa.
Leave a Comment