Maafisa watatu wa polisi wanaofanya kazi katika kituo cha jogoo wamekamatwa kwa madai ya kusaidia katika kutoroka kwa mshukiwa wa mauaji Masten Millimo Wanjala hapo jana.
Watatu hao ni Inspekta wa polisi Philip Mbithi na makostebo Boniface Mutuma na Precious Mwende.
Watatu hao waliokamatwa na kitengo cha upelelezi wa jinai kaunti ya Nairobi, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo.
Watashtakiwa kwa kumsaidia mshukiwa aliyekiri kutekeleza mauaji kutoroka, pamoja na kutelekeza majukumu yao.
Wanjala ambaye alikiri kuua wasichana wasiopungua kumi, alitoroka kutoka seli za kituo cha Jogoo hapo jana Okt 13, wakati alikuwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani kukabiliwa na mashtaka 13 ya mauji.
Leave a Comment