Maafisa wa polisi wa kituo cha Embakasi kule Nairobi wanamzuilia mwanamke anayedaiwa kushirikiana na kijana kutapeli mumewe kwa kujifanya kwamba ametekwa nyara.
Washukiwa hao Jane Wairimu na Richard Mogire (21) wanasemekana kupanga njama ya kumtapeli Brian Mutuku.
Kulingana na DCI, Wairimu alitoweka siku ya Ijumaa wiki jana na kuacha mumewe na wasiwasi tele.
Usiku huo wa Ijumaa Mutuku alipokea simu kutoka kwa mkewe ambaye alimuarifu kwamba alikuwa ametekwa nyara na watu ambao walikuwa wanataka kulipwa shilingi laki mbili ili awachiliwe.
Mutuku pamoja na familia ya Wairimu waliweza kuchanga shilingi 17,000 na kutumia ‘watekaji nyara’ wale ili kujaribu kuwashawishi wamuachilie.
Kuona kwamba Wairimu hakuwa anarejea nyumbani, familia yake iliunda kikundi cha WhatsApp na wakachanga shilingi 40,000 zaidi ambazo waliwatumia ‘watekaji nyara’ wale siku ya Jumatatu.
Kufuatia hayo mume wa mshukiwa alipiga ripoti katika kituo cha DCI cha Embakasi kwamba mkewe alikuwa ametoweka na uchunguzi kuanzishwa.
DCI imebaini kuwa watatu hao wamekuwa wakikaa pamoja tangu siku ya Jumatatu hadi jana ambapo walikamatwa katika maeneo ya Sagana.
Leave a Comment