Serikali imekana madai ya kuwa kemikali zilizotumiwa kwenye mtihani wa kemia wiki jana zilikuwa na sumu iliyowaadhiri baadhi ya wanafunzi kote nchini.
Katibu wa kudumu katika wizara ya elimu Dkt Belio Kipsang amesema kuwa kemikali hizo ni zile za kawaida ambazo pia zimekuwa zikitumiwa na wanafunzi katika masomo yao ya kawaida.
Akizungumza baada ya kuzuru shule za upili ya Milimani na ile ya Naivasha Girls, Kipsang vile vile amesema serikali inachunguza ripoti kuwa wanafunzi kumi kutoka shule ya Milimani hawajafanya mtihani huo licha ya kujisajili.
“Hakujakua na maafa yoyote ,wiki iliyopita nilitembelea shule kadhaa ,kemikali hizi ni zile amabazo wamekua wakizitumia shuleni.Hadi wiki hii hakuna mwananafunzi ambaye ameripoti kuharibikiwa na kemikali hizo ila serikali itachunguza jambo hili.”Amesema Dkt Belio Kipsang’
Silas Mwiti
Leave a Comment