Mwanaume mmoja amemuua mkewe kwa kumdunga kisu katika ploti moja karibu na shule ya msingi ya wasichana ya St. Mary’s karibu na uwanja wa michezo wa Afraha mjini Nakuru usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa polisi eneo bunge la Nakuru Mashariki Hellena Kabukuru alithibitisha hayo akisema kuwa mshukiwa Paul Ochieng’ mwenye umri wa miaka 40 alikuwa na ugomvi na mkewe Njeri Kamande mwenye umri wa miaka 27 kabla ya kumdunga kisu na kufa papo hapo.
Ilibainika kuwa, mwanaume huyo alijaribu kuruka kutoka ghorofa ya nne ya jumba hilo kabla ya majirani kumkamata na kumkabidhi mikononi mwa polisi.
Mwili wa marehemu upo katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya kaunti ya Nakuru.
Leave a Comment