Serikali ya kaunti ya Nakuru imesema itaongezea kilimo cha pareto mara dufu katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Kulingana na waziri wa kilimo wa kaunti ya Nakuru Dkt Immaculate Maina, wanashirikiana na kampuni ya marekani ya KENTEGRA ili kufanikisha kilimo cha pareto huku wakinuia kuongezea ekari mia saba kutoka kwa ekari elfu mbili zinazolimwa.
Maina anasema kuwa tayari serikali imetenga shilingi milioni 25 zitakazotumika kuimarisha kilimo hicho kwa kununua mbegu zitakazopewa wakulima.
Akizungumza eneo la Eburru kaunti ndogo ya Gilgil, Maina amesema kampuni hiyo imeonyesha nia ya kununua pareto kwa wakulima kila baada ya wiki mbili na kuwalipa wakulima kwa wakati unaofaa.
NA SILAS MWITI
Leave a Comment