Afisa mmoja wa polisi kwa jina Donald Rutto kutoka kaunti ya Wajir, anazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Menengai Magaribi kaunti ndogo ya Rongai hapa Nakuru, akishukiwa kuhusika na mauji, baada yake kujisalimisha mapema leo.
Kwa mujibu wa OCPD wa Rongai Richard Rotich, Rutto anashukiwa kushirikiana na mkwewe Anita Njeri ambaye alikuwa amekamatwa hapo awali, kwa mauaji ya Teresia Njangogu eneo la Ol-rongai siku ya Jumamosi.
Kulingana na Rotich, afisa huyu wa polisi alikuwa kwenye likizo ya siku 14 iliyoanza tarehe 8 mwezi huu na kutarajiwa kukamilika 25 wiki hii.
Afisa huyo wa polisi ndiye anadaiwa kupiganiwa na wanawake hao wawili, kwenye mzozo wa kimapenzi na anatarajiwa kusaidia kwenye uchunguzi dhidi ya kesi hii.
Teresia Njangogu alipatikana amefariki siku ya Jumamosi wikendi ambayo imepita kwenye eneo la Ol-Rongai, huku mwili wake ukiwa na majeraha makali.
Leave a Comment