Gari la polisi kutoka kituo cha polisi cha Timboroa limehusika katika ajali karibu na kituo cha biashara cha Total kwenye barabara kuu ya Nakuru-Eldoret.
Kwenye ajali hiyo watu 4 wamenusurika kifo baada ya karandinga hiyo ya polisi kugongana na gari ndogo.
Gari hilo lililokuwa limebeba mahabusu linasemekana kuendeshwa kwa kasi kabla ya kuyapita magari mengine matatu na hatimae kupoteza mwelekeo.
Maafisa wa polisi kutoka Mau Summit wameanzisha uchunguzi wa ajali hiyo.
Leave a Comment