Kamati ya usalama eneo bunge la Bahati ikiwemo OCPD wa Bahati Bernard Wamugunda, Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Bahati Godfrey Mayama, naibu kamishna wa eneo la kiamaina, OCS wa kituo cha polisi cha Kiugu-ini Solomon Wamae, chifu wa Hodi Hodi na manaibu wake wamesimamishwa kazi kwa muda kufuatia matukio ya pombe haramu yaliyopelekea maafa ya watu kumi katika eneo bunge la Bahati wiki jana.
Akizungumza na wanahabari mratibu wa eneo la bonde la ufa George Natembeya amesema maafisa hao wana siku 21 kujieleza kuhusiana na kisa hicho.
Aidha Natembeya amewapa maafisa wa usalama wanaozembea kazini kuwa chuma chao ki motoni.
Leave a Comment