Wakaazi wa kaunti ya Narok wanaotoka jamii za wafugaji wamehimizwa kukumbatia elimu ili kufanikisha maendeleo maishani mwao. Hayo ni kulingana na kasisi wa kanisa la katoliki Francis Kregerler kutoka John Bosco ambaye amezungumza katika viunga vya mbuga ya wanyamapori ya Maasai Mara akidai ipo haja ya kuasi ukeketaji na ndoa za mapema kwa watoto wa kike.
“Elimu ndio nguzo ya jamii,lazima tuipende na kuwaruhusu wanafunzi waende shuleni ili katika maisha ya usoni tuwe na mwelekeo.”Akasema Francis Kregerler
Aidha, Kregerler amehimiza jamii isimbague mtoto wa kiume kwani waume wana uwezo wa kubadili mtazamo hasi dhidi ya mtoto wa kike kielimu.
Himizo pia lilielekezwa kwa viongozi kwa kuzidisha fedha za kuwafadhili wanafunzi kutoka familia zisizojiweza kiuchumi.
Leave a Comment