Mshirikishi wa kanda ya bonde la ufa George Natembeya amesema kuwa vita vya utovu wa usalama vinavyoshuhudiwa katika eneo la Laikipia havitokani na malisho bali mizozo ya mashamba na kuwa baadhi ya viongozi nchini wanahusishwa.
Natembeya, amesema watu wanane, wakiwemo polisi watatu, ndio wamepoteza maisha katika muda wa mwezi mmoja kutokana na vita vya kule Laikipia.
Wanauguza majeraha ni raia wanne na polisi wawili, Natembeya akikanusha taarifa kwamba darasa liliteketezwa wakati oparesheni ya polisi ikiendelea.
Leave a Comment