Wingu la simanzi limetanda katika Kijiji cha Kirimangai kule Kasuku kaunti ya Nyandarua baada ya ajuza (99) kuteketezwa na Moto kiasi Cha kutotambulika leo alfajiri.
Kulingana na ripoti ya polisi, mabaki ya mwili wa ajuza huyo kwa jina Ruth Munyive Mwinde yalipelekwa katika makafani ya hospitali ya J.M Kariuki huku uchunguzi wa kiini cha Moto huo ukianzishwa.
Familia
ya ajuza huyo ambayo imezungumza na kituo hiki kwa njia ya simu imesema ukosefu wa maji katika eneo hilo ulifanya
juhudi za kuuzima moto huo zisifue dafu.
Leave a Comment