Bunge la kaunti ya Nyandarua limefungwa kwa mda wa siku kumi na nne kufuatia maambukizi ya virusi vya Corona katika bunge hilo.
Naibu spika wa bunge hilo, Zachary Njeru, amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuzuia maambukizi zaidi ya wimbi la Delta Variant bungeni, shughuli za kamati zikitakiwa sasa kuendelezwa mitandaoni.
Aidha Njeru amewahimiza wawakilishi wadi pamoja na wafanyakazi katika bunge hilo kutumia mda huo wa siku kumi na nne kuchanjwa na kuwahamasisha wakazi wa kaunti ya hiyo kupokea chanjo.
Leave a Comment