Wizi wa vifaa vya umeme vimetajwa kuwa chanzo kuu cha ukosefu wa umeme katika baadhi ya maeneo ya kaunti ya Nyandarua.
Licha ya serikali kujitahidi kuhakikisha wakazi wengi katika kaunti ya Nyandarua wameunganishwa na umeme wahalifu wa vifaa muhimu vya umeme mathalan transfoma au ufyonzaji wa mafuta yake wamekuwa kero kubwa kwa jamii inayofaidi umeme katika kaunti hiyo.
Katika eneo la Mwireri Olkalou transfoma moja imeharibiwa na watu wasiojulikana huku wafanyakazi katika ofisi ya mbunge wa eneo hilo wakiwahimiza wakaazi kuwa macho na kuripoti uhalifu wa aina yoyote ya stima.
Leave a Comment