Wanafunzi zaidi ya 7,000 katika eneo bunge la Olkalou kaunti ya Nyandarua wanakila sababu ya kutabasamu baada ya mbunge wa eneo hilo David Kiaraho kuwapa basari milioni takriban 30.
Akizungumza katika eneo la Milangine wakati wa kupeana basari hizo, Kiaraho alikashifu mgogoro ambao umekuwepo Katika kaunti ya Nyandarua Kati ya bunge na uongozi wa kaunti hiyo.
Kiongozi huyo alisema mvutano huo umewafanya wanafunzi kukosa basari za kaunti na vile vile kukosekana kwa fedha za maendeleo.
Leave a Comment