Wakulima wa mifugo katika eneo la Mumui Kipipiri Kaunti ya Nyandarua wameendelea kukadiria hasara baada ya fisi kuvamia mifugo yao mara kwa mara.
Wakaazi hao wamesema kuwa ni Jambo la kutia hofu kwani usiku wa kuamkia leo fisi waliwavamia ng’ombe wawili wa maziwa na kuwaacha na majeraha makubwa.
Wakazi hao Sasa wamewataka maafisa wa kulinda wanyamapori kuwadhibiti fisi hao ambao wameendelea kuwahangaisha, wasije wakakadiria hasara zaidi au hata kuwapoteza mifugo.
Leave a Comment