Vijana katika eneo la Baringo sasa wanahimizwa kukumbatia fursa za mikopo ambayo hutolewa na serikali kwa manufaa yao, ili waweze kuboresha maisha yao.
Akihutubu katika eneo bunge la Mogotio ambapo alizindua zoezi la kugawa vyakula vya msaada mnamo Jumanne, msemaji wa serikali Kanali mstaafu Cyrus Oguna alisema idadi kubwa ya vijana wamezidi kupuuza hazina ya uwezo ambayo ilibuniwa na seikali, ili kuwasaidia kupata mikopo kwa njia rahisi na haraka.
“Wakati wa zamani ilikuwa vigumu kupata mikopo kwenye benki, ila kwa sasa serikali imetoa njia kama Uwezo Fund ambayo inalenga kusaidia wakenya kupata mtaji wa haraka kuanzisha biashara” Oguna akasema.
Aidha Oguna alitoa wito kwa maafisa wanaosimamia hazina hiyo kuchukua hatua za dharura, na kuhakikisha kwamba fedha kwenye hazina hiyo zinafikia makundi ya vijana ambayo yanafaa kuwa wafaidi.
Na Jeremiah Chamakany
Leave a Comment