Polisi siku ya alhamisi walianzisha uchunguzi kuhusiana na mauaji ya afisa mmoja wa polisi aliyepigwa risasi kwenye mtaa wa Kayole jiji Nairobi.
Afisa huyo kwa jina David Maya wa kitengo cha DCI,alikuwa na mkewe wakati wa mauaji hayo na Kulingana na mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei, wawili hao walikuwa wameegesha gari lao kwenye sehemu ya Hurlingham huko Kayole kurekebisha gurudumu,wakati walipovamiwa na watu watatu waliokuwa kwenye piki piki na kumpiga risasi kichwani huku mkewe akijeruhiwa kwenye mguu wake.
Tukio hilo aidha lilinaswa kwenye kamara za CCTV.
Mwili wake ulihifadhiwa na unasubiri kufanyiwa uchunguzi katika hospitali moja Jijini Nairobi.
Leave a Comment