Kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa mara nyingine ameikashifu bunge kwa kukosa nguvu dhidi ya serikali kwa kupitisha sheria zinazowakandamiza wananchi wa kenya.
Akizungumza huko Vihiga,Odinga pia amemkashifu Rias William Ruto kwa kukosa kuheshimu idara ya mahakama.
Raila alitoa mfano wa muungano wa azimio ulipoheshimu uamuzi wa Mahakama dhidi yao katika kesi waliyowasilisha kupinga ushindi wa rais ruto katika uchaguzi wa mwaka 2022.
Odinga sasa amemtaka jaji mkuu Martha Koome kutofanya mazungumzo na Rais William Ruto akidai kuwa hali hiyo ni hujuma kwa sheria na mahakama.
Leave a Comment