Serikali ya kaunti ya bungoma yalaumiwa kwa kuwanyima ufadhili wa karo wanafunzi wanaojiunga na shule za ipili kutoka jamii maskini na pia wakiwemo waliopata zaidi ya alama mia nne
Utata unaizingira serikali ya kaunti ya bungoma hii ni kuhusiana na ufadhili wa karo ya wanafunzi wanaojiunga na shule za ipili kutoka jamii maskini na pia wakiwemo waliopata zaidi ya alama mia nne
Hali hii imelazimu vuguvugu moja linalotetea haki za kibinadamu la Bungoma Liberation likiongozwa na Zacharia Barasa kujitolea na kuwalipia karo zaidi ya wanafunzi arobaini kutoka familia maskini wakiwemo yatima waliopata alama mia moja za zaidi
Barasa akishinikiza kwamba sio vema wanafunzi kama hao kuachwa nje ikizingatiwa kwamba wazazi wao hawajiwezi ni kumaanisha wengi wao masomo yao hukatizwa
Leave a Comment