Nakuru 1pm December 5, 2019
Taasisi ya Rift Valley Institute of Science and Technology RVST imepata afueni kwenye ombi lao la kuhifadhi kipande cha ardhi ekari 2700 baada ya mahakama ya ardhi na mazingiria kupuzilia mbali hati miliki zinazodaiwa kupatikana kiharamu.
Kwenye kesi iliyowasilishwa mbele ya Jaji Silas Munyao na uamuzi wake kutolewa na jaji Dalmas Ohungo ni kuwa hamna ushahidi wowote kuwa ‘Trustees’ walio na jukumu la kuunga mkono kuuzwa kwa ardhi walikubaliana kwa vyovyote kuhusiana na kununulia kwa ardhi hiyo .
Ardhi hiyo inamiliki taasisi hiyo ya RVST sawa na shamba lake huku trustees hao wakisema ilikuwa imekatwa vipande na kuuziwa wawekezaji wa kibinafsi.
Jaji Ohungo katika uamuzi wake akisema vipande hivyo havikuchuliwa kwa njia ya kisheria na kihaki na kuamrisha virejeshwe katika ardhi ya taasisi hiyo.
Julius Sunkuli ni katibu wa ‘Trustees’ hiyo na amesema imekuwa kipindi kirefu tangia mwaka 2006 kupata hki kwao kuhusina na kipande hicho cha takriban hekari 6000.
Leave a Comment