Mwakilishi wadi ya Tenges kwenye bunge la Baringo Silas Tochim ameshutumu serikali kwa madai ya kukosa kutekeleza usawa katika maeneo ya Baringo ambako wananchi wameendelea kuathirika na janga la utovu wa usalama.
Akihitubu katika hafla moja ya hadhara katika kaunti ndogo ya Eldama Ravine, Tochim alisema serikali ilichukua hatua za dharura kujenga nyumba kwa wakaazi wa maeneo ya Laikipia ambapo utovu wa usalama ulishuhudiwa, lakini ilifeli kujenga nyumba kwa wakaazi wa Baringo ambapo wakaazi walioathirika wanaishi kama wakimbizi.
Aidha, Tochim alisema serikali ni sharti izingatie haki na usawa kwa wakenya wote na hasa kwa kukimu maslahi ya wakimbizi.
Leave a Comment