Viongozi kutoka kauti ya Elgeyo Marakwet wamesema kuwa wataenda kukumbatia misafara ya amani katika juhudu za kuhakikisha kuwa amani imedumishwa katika maeneo ya Kerio Valley.
Wakiongozwa na seneta wa kaunti hiyo Kipchumba Murkomen , viongozi hawa wamesema kuwa hatua hiyo itaenda kuwawezesha wakazi kuishi kwa amani.
Murkomen ameongeza kuwa kwa muda wa miezi mitano sasa wakazi wameweza kuishi kwa amani.
Murkomen vile vile amesema kuwa serikali imejisatiti kuona kuwa miradi mbali mbali za maendeleo zimetekelezwa katika maeneo hayo hivyo basi wakazi wanapaswa kutumia fursa hiyo kujiendeleza.
Haya yanajiri baada ya maombi ya amani ya kila mwaka kufanyika katika eneo la Kapsait mpakani mwa kaunti ya Elgeyo Marakwet na Pokot magharibi.
BETRICE KOECH
Leave a Comment