Wazazi wametakiwa kuwa kwenye mstari wa mbele katika kukutea haki za watoto, dhidi ya watu ambao wamekuwa wakiwadhulumu watoto haswa wa jinsia ya kike kimapenzi.
Hii ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake kwenye kaunti ya nakuru eunice lelei, ambaye amesema kwamba,kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la visa vya ubakaji katika maeneo ya rongai,sowin na solai,ambavyo husuluhiswa vijijini bila ya kuripotiwa kwenye vituo vya polisi au hata afisi za watoto.
Kulingana na Lelei,serikali inapaswa kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi ambao wamekuwa wasuluhisha kesi hizi mashinani, badala ya kuwakinga watoto wao dhidi ya watu ambao wanawanyanyasa na kuharibu maisha yao.
Leave a Comment