Maafisa wa upelelezi nchini DCI wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa cha kuangamizwa kwa Jamaa mmoja aliyedungwa kisu kifuani kufuatia mzozo wa kazi .
Kulingana na DCI, Peter Ekai (30) na Elphas Kipkoech (26) walikuwa wanalewa kwenye baa moja katika eneo Longisa, Bomet wakati mzozo huo ulitokea.
Vile vile DCI inasema wawili hao walitofautiana baada ya Ekai kudai kwamba Kipkoech alikuwa anapanga njama ya kumpokonya kazi yake ya ulinzi katika shirika moja la usalama lililo maeneo ya Kamagut.
Kutokana na mvutano huo wawili hao walianza vita vya silaha zenye makali na kudungana kabla ya Ekai kuumia vibaya kwani alidungwa kwenye kifua na kukimbizwa katika hospitali ya Moi Teaching and Referral ambako aliangamia.
Kipkoech ambaye pia alijeruhiwa, alihudumiwa kwenye hospitali iyo hiyo na kuruhusiwa kuenda nyumbani kabla ya kukamatwa na polisi na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Eldoret.
Mshukiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani kushtakiwa kwa mauaji.
Leave a Comment