Mwakilishi wa kina mama kwenye kaunti ya Nakuru Liza Chelule, amewataka kina mama na vijana kukumbatia mikopo ya fedha za hazina ya Uwezo, ambazo hutolewa na serikali kuu.
Akiongea kwenye mkutano ulioyaletafedha pamoja makundi mbalimbali ya kina mama kwenye wadi ya Lanet, Chelule amewataka kina mama na vijana pamoja na watu wanaoishi na ulemavu, kutumia fedha hizo kikamilifu ili waweze kujiendeleza kupitia biashara mbalimbali.
Wakati huo huo, amewarai viongozi pamoja na wananchi kuhakikisha wanadumisha amani katika maeneo bunge yao na kaunti kwa ujumla.
Warukira Mwangi
Leave a Comment