Viongozi mjini Naivasha wamekaribisha hatua ya kuanzishwa kwa eneo maalum la viwanda huko Mai mahiu na kusema kutaleta manufaa makubwa kwa wakazi.
Aliyekuwa mbunge wa eneo hilo John Mututho amewaongoza viongozi wengine kwa kusema eneo hilo na ambalo ujenzi wake sasa umekamilika utabadilisha maisha ya mji huo na kuinua uchumi wake.
Mututho amesema sasa kulikuwa na haja ya kuwekwa mipangilio mwafaka eneo hilo ili kuweza kuwa na nafasi za kupitishia maji ya mafuriko tukio litakalopelekea ongezeko la wawekezaji.
Naye naibu wa kamishna wa kaunti ndogo ya Naivasha Mbogo Mathioya amesema barabara ya kuelekea eneoo hilo tayari imekamilika na sasa wanasubiri kufunguliwa rasmi ili shughuli zianze.
Leave a Comment