Wakaazi wanaoishi maeneo yanayopakana na kaburi la Njoro la Kang’ari wanaishi kwa hofu kufuatia mvua nyingi na mafuriko wanayosema yanaweza kufukua na kufanya miili kwenye kaburi hilo kuelea.
……huku hayo yakijiri
Mwalimu mmoja mwenye umri wa miaka 37 wa shule ya upili huku Njoro amekatakatwa hadi kufa na jamaa mmoja kufuatia kile kinaaminika kuwa mzozo wa shamba eneo la Tuyoibei Emitik huko Kuresoi Kusini.
Kulingana na chifu wa Emitik David Cheruiyot, mwalimu huyo alifika kwenye shamba lake na kutofautiana na jamaa wanayepakana katika shamba hilo tukio lililopelekea jamaa huyo kumkatakata mwalimu huyo kwa upanga aliokuwa nao.
Juhudi za wananchi hata hivyo za kumkimbiza hospitalini Mwalimu huyo hazikufua dafu kwani aliaga dunia alipofikishwa kwenye kituo cha matibabu cha Olenguruone.
Chifu Cheruiyot anasema mshukiwa ambaye amekamatwa na polisi amekuwa na mizozo na watu wengi katika eneo hilo.
Leave a Comment