Wakaazi wa kutoka eneo la Murunyu walifanya maandamano Jumanne adhuhuri na kufungua barabara ya Murunyu kuelekea Mawanga katika kaunti ndogo ya Bahati hapa Nakuru, wakidai kwamba ujenzi wa barabara hiyo ambao unaendelea umesababisha kuharibiwa kwa mifereji ambayo husambaza maji kwenye boma zao.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wakaazi hao wamedai kupatwa na kiu kutokana na ukosefu wa maji kwa muda wa miezi 3 sasa, huku wakiitaka kampuni ya usambazaji maji Nakuru NARUWASCO kuangazia swala hilo.
Wakiongozwa na Paul Thiong’o, wakaazi hao wameisuta kampuni hiyo kwa kuwatumia bili za kulipa maji ilhali maji yenyewe hawaipati.
“Kwa miezi Mitatu sasa hatuna maji. Tunaenda kilomita sita kutafuta maji ili tupate ya kutumia”, Thiong’o akasema, huku kampuni ya NARUWASCO ikisalia kimya kuhusu madai hayo.
Na Miriam Itotia
Leave a Comment