Muungano wa mataifa ya Bara Uropa umetoa jumla ya shilingi milioni mia moja unusu zitakazotumiwa kuwasaidia wakulima ili kuimarisha mazao yao.
Kwenye mradi wa miaka mitatu, muungano huo utatoa fedha kwa shirika la WWF ambalo litafanya kazi kwa karibu na wakulima ili kuweza kutimisha lengo lao.
Akizungumza eneo la Ndabibi mjini Naivasha, Balozi wa muungano huo nchini Kenya Simon Mordue, kaunti tatu zitanufaika na mradi huo huku wakulima wakipata mbegu za kisasa na mafunzo ya kuweza kuboresha kilimo chao.
Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la WWF Mohammed Awer amesema kaunti za Nyandarua, Nakuru na Narok zitanufaika na mradi huo wa miaka mitano.
Leave a Comment