Takriban wanabiashara 5 kutoka kituo cha kibiashara cha salgaa wanakadiria hasara baada ya moto kuzuka jana usiku na kuteketeza maduka yao.
Akizungumza na kituo hiki usiku wa kuamkia leo mwenyekiti wa nyumba akumi kata ya salgaa Andrew Koros amesema kwamba,moto huu unashukiwa kuanzia kwenye duka moja la vibanzi na mwishowe kusambaa hadi kwenye maduka mengine.
Ameongeza kuwa,kuchelewa kwa gari la kuzima moto la kaunti ya nakuru,ndiko kulipelekea hasara zaidi kushuhudiwa.
Akidhibitisha kisa hiki Ocpd wa Rongai Richard rotich ametaja kuwa,bado chanzo cha moto hakijaweza kubainika,kwani juhudi zote zilikuwa za kujaribu kuuzima moto huo……..Kwingineko
Mfanyabiashara mmoja kutoka mji wa Olkalou kaunti ya Nyandarua amewashangaza wengi baada ya kuandikia rais Uhuru Muigai Kenyatta hundi ya shilingi 10,500 kama mchango wake katika vita dhidi ya ugonjwa wa Covid -19.
David Wanjohi wamesema kuwa ni jukumu la kila mmoja haswa wanaojiweza katika taifa hili kusaidia wanyonge na wasiojiweza wakati huu mgumu wanapokabiliana na ugonjwa wa Covid- 19.
Leave a Comment