Raia wa Zambia wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais ambao kura za maoni zinaonesha utakuwa kinyang’anyiro kikali kati ya rais Edgar Lungu na mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema.
Hichilema mwenye umri wa miaka 59, anagombea kwa mara ya sita na amewahi kushindwa mara mbili na Lungu, mara ya kwanza katika uchaguzi wa 2015 baada ya kifo cha rais wa zamani Michael Sata na katika uchaguzi mkuu uliofuata mwaka mmoja baadaye. Kuna wagombea kumi na sita wa nafasi ya urais.
Lungu, mwenye umri wa miaka 64 alilituma jeshi kuzima machafuko yaliyoibuka baada ya makabiliano kati ya wafuasi wa vyama vianavyohasimiana kuelekea uchaguzi wa leo wa rais na bunge, hatua iliyokosolewa na wakosoaji kama mbinu ya kuwatisha na kuwahujumu wapigaji kura wafuasi wa upinzani.
Leave a Comment