Washikadau wa ziwa la Naivasha wameelezea wasi wasi wao kutokana na kiwango kikubwa cha maji yanayotolewa ziwa hilo kutumika katika shuguli za ujenzi na kilimo kila siku.
Wakuu hao wamesema kuwa mradi wa kupeleka maji katika eneo kunakojengwa viwanda na bandari kutaadhiri pabaya kingo za maji ya ziwa hilo.
Kulingana na mwenyekiti wa washika dau hao Enock Kiminta, ziwa hilo linapoteza mamilioni ya lita za maji kila siku.
Akizungumza wakati wa mkutano wa muungano wa washika dau hao katika hoteli moja mjini Naivasha, Kiminta amesema kampuni za maua na shirika la Kengen zinaongoza katika uchotaji maji hayo kwa wingi hatua ambayo inafaa kukomeshwa.
Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Imarisha Naivasha Kamau Mbogo amesema kuwa kiwango cha maji kilichokuwa kikingia kwenye ziwa hilo kimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na ukosefu wa mvua katika maeneo ya vyanzo vya maji vya ziwa hilo.
Leave a Comment