Aliyekuwa naibu waziri wa habari na mawasiliano katika serikali ya awamu ya tatu, Koigi Wa Wamwere amesema ili kukabiliana na kirusi cha Corona, rais Uhuru Kenyatta angestahili kuweka mikakati zaidi ya kupambana na virusi vipya vya Omicron ili kuzuia visiingie nchini.
Koigi alisema hayo leo asubuhi kupitia kituo hichi, kipindi cha Maskani kitengo cha kero nyeti, akisema hotuba ya rais ilikuwa ya kujitafutia sifa na wala si kusuluhisha matatizo yanayowakabili wakenya.
Kando na ungozi mbaya, Koigi alisema rais alihitaji kuangazia ufisadi, umaskini na ukabila, kwenye hotuba yake.
Wakati uo huo Koigi alikosoa hotuba kuhusu maendeleo ya Kenya na yale yaliyoko katika mataifa ya bara Asia yaliyofanikiwa kuafikia upeo wa maendeleo kwa muda mfupi.
Kulingana na Koigi, uongozi mbaya ndio umesababishia Kenya ukosefu wa maendeleo na bila kuondokana na uongozi huo, Kenya haiwezi kupata maendeleo kama yaliyoko mataifa ya bara Asia.
Leave a Comment