Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi atawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama cha Democratic, DP.
Tangazo hilo lilitolewa mjini Nyeri wakati wa mkutano wa wajumbe wa chama hicho katika eneo la mlima Kenya, ulioongozwa na mwenyekiti wa kitaifa Esau Kioni siku chache baada ya Muturi kuahidi kuweka wazi chama atakachokitumia kuwania urais mwaka ujao.
Kwa mujibu wa chama hicho, Muturi ndiye kiongozi atakayeleta mabadiliko yanayosubiriwa kwa hamu na wakenya.
Muturi ameahidi kushirikiana tu na viongozi walio na mawazo sawa na yake.
Thank you for the good work