Mwanasiasa Koigi Wa Wamwere amesema uchaguzi mkuu uliopita ulishuhudia idadi ndogo ya wapiga kura ikilinganishwa na chaguzi za hapo awali.
Akizungumza na kituo hiki cha sauti ya mwananchi kwenye kipindi cha Cheche,Koigi alisema kuwa ingawaje haijabainika ni kwa nini, idadi hiyo ilikuwa ya chini mno,waliosusia walikosa kutoa sauti yao katika kuwachagua viongozi wanaowataka.
Wakati uo huo,Koigi aliipongeza tume ya IEBC kwa kuweka wazi matokeo yake kwa kuhesabu kura peupe lakini hata licha ya hayo,mwanasiasa huyo alidai kuwa baadhi ya mawakala wake walifungiwa nje katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.
Kiongozi huyo pia alidai kuwa kuna baadhi ya wawaniaji waliopoteza kura baada ya mchakato mzima kuborongwa.
Kuhusiana na uadilifu wa makamishna wa IEBC,mwanasiasa huyo alisema ni muhimu kwa maafisa hao kuwa waadilifu zaidi kwa sababu ya kazi yao.
Hata hivyo aliwasuta baadhi ya makamishna wa IEBC kwa kufeli kuafikiana katika hesabu za kura za urais akidai kuwa huenda kulikuwa na ufisadi kati ya maafisa hao wa tume ya uchaguzi.
Leave a Comment