Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru amefichua kwamba hawezi kufutilia mbali uwezekano wa kufanya kazi na naibu rais dkt William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2022.
Hata hivyo Waiguru amesema kuwa bado ni mapema sana kuzungumzia suala la iwapo anaweza kujiunga na UDA au atasalia kwenye jubilee.
Gavana huyo alifunguka kuhusu mipango yake ya kisiasa ya 2022 akisema kwamba hata kama hawezi kutangaza wazi iwapo atajiunga na UDA, watu wa Kirinyaga ndio watafanya maamuzi ya mwisho.
Hivi karibuni gavana Waiguru amekuwa akionyesha dalili za kubadili mkondo wake wa kisiasa haswa baada ya mahakama kutupilia mbali mchakato wa BBI.
Leave a Comment