Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amekiri kuwa kutetea kiti chake kwa tiketi ya Jubilee itamgharimu pakubwa kama uchaguzi ungeandaliwa leo iwapo maswala yanayokisibu chama hicho hayawezi kutafutiwa suluhu la kuokoa meli hiyo inayoongozwa na rais Uhuru Kenyatta.
Akizungumza kwenye runinga moja ya hapa nchini asubuhi ya leo, amesema uchaguzi ungelifanyika leo, Jubilee ingelijipata chini ya tatizo kubwa la kukabiliana na vyama vingine vya kisiasa au hata kuaminisha wakenya kuhusu sera zake.
Gavana Waiguru alisema eneo la mlima Kenya halijafurahishwa na namna chama hicho kimekuwa kikiongozwa kwa miaka mitano iliopita.
Waaidha, Waiguru alisema chama hicho kutokana na umaarufu wake na utendakazi wa serikali haswa kwenye miundo msingi, kingali na nafasi ya kujiokoa.
Leave a Comment