Klabu ya Chelsea haitampiga kalamu kocha Graham Potter hata akikosa kufuzu kwa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.
Uongozi wa Chelsea hata hivyo unalenga kuganda na Potter kwa muda mrefu na hautamtimua asipomaliza ndani ya nne bora kwa kuwa wanalenga kumaliza utamaduni wa kuwapiga makocha kalamu kila mara.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Stamford Bridge, Potter atahudumu kwa muda mrefu kama kocha wa Chelsea mradi tu mambo yanaenda vizuri hata iwapo ni kwa kasi ya chini. ….Potter ambaye alitwaalia Alhamisi, Septemba 8, kutoka Brighton anajua kigezo cha chini kabisa cha ufanisi katika klabu ya Chelsea ni kufuzu kwa michuano ya klabu bingwa.
Chini ya aliyekuwa mmiliki Roman Abrahimovich, klabu bingwa iliamua kwa kiasi kikubwa hatima ya kocha lakini wamiliki wapya Todd Boehly na Behdad Eghbali wanataka kubadili utamaduni huo.
Leave a Comment