Leo usiku anga za bara ulaya zitaendelea kupolea kisoka kufuatia ratiba ya ligi ya UROPA na ile ya KONGAMANO.
Michuano inayopewa kipaumbele kwenye ligi ya kongamano ni ile ya saa mbili kasorobo usiku mchanga, Tottenham kutoka Uingereza dhidi ya Stade Rennais kutoka Ufaransa na ule wa saa nne usiku, Roma kutoka italia akiwa nyumbani dhidi ya CSKA Sofia kutoka Bulgaria.
Katika ligi ya Uropa saa mbili kasorobo usiku mchanga, Westham wa Uingereza watapambana ugenini dhidi ya Dinamo Zagreb ya Kroatia huku saa nne usiku, Napoli ya Italia wakisafiri hadi Uingereza kukipiga na Leicester City miongoni mwa michuano mingine.
Leave a Comment