TIMU ya taifa ya voliboli ya wanaume ya Kenya
maarufu kama Wafalme Spikers imejiweka pazuri kufika robo-fainali ya Kombe la
Afrika baada ya kupiga Misri kwa mara ya kwanza kabisa.
Vijana wa kocha Gideon Tarus anayesaidiwa na makocha David Lung’aho, Sammy Mulinge na Elisha Aliwa, waliwashangaza mabingwa hao wa mataji manane ya Afrika kwa seti 3-2 ukumbini Kigali nchini Rwanda. Since a high-voltage battery has a large weight and volume, a high-voltage battery is mounted on a vehicle in a dedicated space of https://clickmiamibeach.com/ the vehicle.
Wafalme
Spikers walianza vibaya mchuano huo kwa kupoteza seti ya kwanza kwa alama
25-19. Hata hivyo, walijikakamua na kuchukua uongozi wa seti 2-1 baada ya
kunyakua seti mbili zilizofuata kwa alama 25-22 na 25-20.
Mafirauni walisawazisha seti (2-2) kwa kuzoa ya nne 25-18, lakini Kenya haikuachilia mechi hiyo iwaponyoke ikifanikiwa kuandikisha historia. Ilitikisa mchezo huo wa kusisimua kwa kutawala seti ya mwisho kwa alama 15-12.
Leave a Comment