repliche orologi replica uhren
Sports/Michezo

Wikendi ya mwenye nguvu mpishe EPL ikipamba moto

UBABE WA LIVERPOOL
Written by admin

Liverpool walijinyanyua upesi na kubebesha limbukeni Bournemouth gunia la magoli 9-0 uwanjani Anfield.

Arsenal wakaendeleza ubabe wao kwa kutandika Fulham 2-1 ugani Emirates na kusalia kileleni mwa jedwali kwa alama 12.

Awali, Manchester United walikomesha rekodi duni ya kupoteza mechi saba mfululizo za EPL ugenini kwa kutandika Southampton 1-0 uwanjani St Mary’s.

Ushindi huo ulikuwa wa pili kwa mabingwa hao mara 20 wa EPL katika mechi nne za ufunguzi wa msimu huu.

Chelsea nao walizinduka na kupepeta Leicester City 2-1 ugani Stamford Bridge huku mabingwa watetezi Manchester City wakitoka nyuma kulima Crystal Palace 4-2 uwanjani Etihad.

Man-City sasa wana alama 10, tatu mbele ya Chelsea na nne kuliko Man-United wanaowazidi Liverpool kwa pointi moja pekee.

Matokeo ya Man-City wanaopigiwa upatu wa kutwaa taji la EPL mara tatu mfululizo, yalichangiwa zaidi na sajili mpya Erling Haaland aliyepachika wavuni mabao matatu.

Nyota huyo raia wa Norway, aliyetokea Borussia Dortmund kwa Sh7.2 bilioni muhula huu, tayari ana mabao sita katika mechi nne za EPL.

Chini ya kocha Jurgen Klopp, Liverpool walifikia rekodi ya Man-United na Leicester mnamo Jumamosi; ya kuandikisha ushindi mnono zaidi katika historia ya EPL.

Klopp alisema ushindi wao ni ishara ya uthabiti wa kikosi chake, kilichoanza msimu kwa sare mbili mfululizo kabla ya Man-United kuwapepeta 2-1 ugani Old Trafford.

Man-United waliwahi kuvuna ushindi wa 9-0 katika EPL mara mbili – dhidi ya Ipswich mnamo 1995 na Southampton mnamo 2020-21.

Vilevile, Leicester wamewahi kuandikisha magoli sawa na hayo dhidi ya Southampton mnamo 2019.

Baada ya kudhihirisha ni wagombezi halisi wa taji la EPL msimu huu, kocha Mikel Arteta ametaka vijana wake wa Arsenal kutolegeza kamba.

Mara ya mwisho waliposhinda mechi nne za kwanza za msimu mpya wa EPL, Arsenal walinyanyua ubingwa wa ligi mnamo 2003-04 na kuambulia nafasi ya pili 2004-05.

Sasa Arsenal watapania kumaliza mwezi Agosti na ushindi katika mechi tano mfululizo, watakapoalika Aston Villa mnamo Jumatano.

Ushindi wa Chelsea dhidi ya Leicester nao ulichochewa na sajili mpya, Raheem Sterling, aliyeagana na Man-City kwa bei ya Sh7 bilioni.

Nyota huyo – pia wa zamani wa Liverpool – alifunga mabao yote mawili yaliyopaisha Chelsea licha yao kumaliza mechi wachezaji 10.

Leicester sasa imepoteza mechi tatu mfululizo baada ya kufungua msimu kwa sare ya 2-2 dhidi ya Brentford uwanjani King Power.

Ni matokeo yanayomzidishia presha kocha Brendan Rodgers ambaye sasa amelimwa mechi tatu mfululizo kwa mara ya kwanza katika miaka minane.

About the author

admin

Leave a Comment

nude pics of weman wrestler with a boner xxnx.vip latina on black porn videos pornos en familia, mom a d son porn how to download from pornhub xxxpor.win axel kane gay porn my hero academia porn comic, my hero academia porn kimberly delgado only fans wifeporn.win backroom casting couch jena sausage party sex scene