Mbunge wa Bahati kimani Ngunjiri amemtaka Raisi Uhuru Kenyatta kuweka wazi kwa wakenya kuhusiana na hatua anazonuia kufanya kuhusiana na swala nzima la kupanda kwa gharama ya maisha nchini.
Akiongea mjini Nakuru Ngunjiri amesema
kuwa mwananchi wa kawaida ndiye anayeumia zaidi kutokana na hali
hii akisema wengi wa wananchi wanahudumu chini ya mapato ya
shilingi mia kwa sasa.
Aidha amesema kuwa uwepo wa madeni makubwa ya nchi za kigeni ni miongoni mwa baadhi ya hali hii akitaja mfano wa deni la nchini uchina anayosema inakandamaiza uchumi wa taifa
“Watu watakula reli kweli ?Rais anafaa kuelewa kwamaba yeye
ndiye aliyechaguliwa na wananchi “Ngunjiri alisema.
Na Sarah Nyangeri
Leave a Comment